|
Tarehe na Muda wa Sasa Wednesday, 18 Dec 2024 - 11:53 (GMT +3) | Hali ya Hewa ya Sasa Wednesday, 18 Dec 2024 @ 11:00 EAT 30°C (86°F) Humidity: 57% Wind: North East 2.1 |
Taarifa za Sarafu Wednesday, 18 Dec 2024 @ 11:00 EAT TZS ~ Tanzanian Shilling 1 USD = TZS 2343.74 | 1 EUR = TZS 2460.26 *Viwango hivyo hapo juu ni baina ya benki/vya kati. Miamala ya pesa taslimu na kadi ya mkopo huenda ikategemea gaharama za juu za mahali husika. |
|
Ambacho kilikuwa kijiji cha wavuvi kitulivu na kinacholindwa kwenye Bahari ya Hindi, Dar es Salaam imekua kwa kasi sana na kuwa Jiji kubwa kabisa la Tanzania na mji mkuu wake wa kibiashara, ni sehemu ya makao makuu ya ofisi za serikali na ofisi za balozi na ngome ya makampuni makubwa ya ndani na ya kimataifa. Kufuatia maendeleo makubwa na ukuaji wake, eneo lake la kimkakati la pwani limelifanya jiji kuendelea na kuwa moja ya kitovu cha biashara Afrika Mashariki chenye ushawishi mkubwa sana. Dar es Salaam pia inasifika kwa kuwa na maeneo na majengo ya kihistoria ambayo yanaonyesha zama zake za kikoloni, huku vivutio vya utalii wa kitamaduni, ikiwa ni pamoja na Makumbusho ya Taifa na Makumbusho ya Vijiji, ambayo hutoa mwanga juu ya makabila ya Tanzania na historia yao ya kupendeza. Migahawa ya kisasa, maduka na migahawa imejaa kwenye mitaa na fukwe nzuri zinapatikana karibu sana na mjini. Hifadhi ya Baharini ya Kisiwa cha Bongoyo kipo km 7 tu Kaskazini mwa jiji na kina maeneo mazuri ya kuzamia na kupiga mbizi na visiwa vilivyojitenga. Jiji hili pia ni lango kuu la kwenda mji wa kihistoria wa Zanzibar, peponi katika Bahari ya Hindi SOMA ZAIDI |