Jengo la kisasa kabisa lenye mwonekano wa kipekee lenye nyenzo bora kabisa katikati ya Kitovu cha Biashara ndani ya jiji liliopo pwani ya Bahari ya Hindi, Johari Rotana inawahakikishia wageni ukaaji wa kifahari usiosahaulika. Sehemu ya eneo la mradi wa MNF Square, yenye maduka makubwa ya bidhaa, makampuni makubwa, karibu na bandari na Feri ya Zanzibar, kitovu cha uchumi, maeneo ya biashara, fuko, na vivutio vingine vikubwa; ni chaguo bora kwaajili ya malazi yasiyo na usumbufu na kwa wasafiri wa kibiashara na starehe, vilevile kwa familia zinazotembelea jiji hili lililochangamka. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere upo umbali wa dakika 30 tu kutoka hotelini na Reli Kuu ipo umbali wa dakika kadhaa.
Imejengwa ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wa kisasa, hoteli hii ya nyota 5 ina vyumba na suite za starehe 193 na vyumba vya kupanga 60 vyenye huduma zote, vikiwa na samani za kisasa, teknolojia na burudani za chumbani za kisasa, na nafasi kubwa zaidi ya kupumzika au kufanya kazi wakati wa ukaaji wako. Iwe una ziara fupi ya kwenda Dar es Salaam au unapanga kukaa kwa muda mrefu jijini hapo, Johari Rotana inatoa aina kadhaa za vyumba ili kukidhi matakwa yako.
Ikiwa ni kula chakula kwa namna tofauti, chagua kutoka kwenye maeneo mazuri matatu au Cigar Lounge, kuanzia mgahawa wa siku nzima wa Zafarani wenye bufee kubwa la vyakula vya Kimediterania, Kihindi, Kiarabu na Kiswahili, hadi Kibo Lobby Lounge kwa ajili ya kahawa na vinywaji, na baa iliyochangamka ya Hamilton’s Gastropub ambapo unaweza kujichanganya, kustarehe na kuvutiwa na vyakula murua vya Kiingereza na Kimarekani. Cigar Lounge inakupa hali ya kifahari na ya kipekee kwa wapenda Cigar katika mandhari ya utulivu na hali ya juu.
Kwa muafaka wa 'kujiweka vizuri', Bodylines Fitness na Wellness Club ni sehemu sahihi ya kupumzika na kuongeza nguvu, ikiwa ni sehemu ya kufanyia mazoezi yenye vifaa vyote, bwawa la kuogelea la nje, ulingo wa mchezo wa ngumi, sauna, vyumba vya mvuke na tiba ya kukanda mwili huku wageni watoto wanaweza kufurahia kwenye klabu ya watoto. Ikiwa unapanga kuwa na mkutano, tukio au hafla maalumu, ikiwa ni pamoja na harusi, ukumbi wetu maalumu wa mita za mraba 2,000 ambao ni ukumbi wa hoteli mkubwa zaidi Dar es Salaam na mkubwa kupita yote Tanzania wenye vyumba sita vya mkutano vyenye vifaa vyote pamoja na zana za sauti na video za kisasa kabisa na mapambo ya kisasa, tunakuhakikisha mikutano ya biashara na ya kijamii yenye mtindo na kijanja.
Tarehe na Muda wa Sasa Sunday, 6 Oct 2024 - 16:33 (GMT +3)
Hali ya Hewa ya Sasa Sunday, 6 Oct 2024 @ 16:00 EAT 28°C (82°F) Humidity: 55% Wind: South East 5.52
Taarifa za Sarafu Sunday, 6 Oct 2024 @ 16:00 EAT TZS ~ Tanzanian Shilling 1 USD = TZS 2736.17 | 1 EUR = TZS 3004.87 *Viwango hivyo hapo juu ni baina ya benki/vya kati. Miamala ya pesa taslimu na kadi ya mkopo huenda ikategemea gaharama za juu za mahali husika.
Sasa Imefunguliwa
Dar es Salaam ni jiji la kibiashara la Tanzania lililochangamka na ndilo Jiji kubwa kuptita yote Tanzania. Lipo katika eneo liliopangwa kimkakati pemebezoni ya pwani ya Bahari ya Hindi, jiji hili, ambalo lilianza kama kijiji kidogo cha wavuvi, limepitia mabadiliko ya kisasa na miaka ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki. Leo bandari yake yenye shughuli nyingi ndiyo bandari kuu Tanzania. Balozi nyingi, vilevile mashirika yasiyo ya kiserikali yapo Dar es Salaam yakiwa yamejiimarisha katika jiji hili lililochangamka, ambalo pia lina migahawa mingi, maduka na majengo ya ofisi.
Masalia ya uwepo wa ukoloni wa Kijerumani bado yanaweza kuonekana katika maeneo na majengo jijini kote. Kuna vivutio maarufu vya utalii kama Makumbusho ya Taifa na Makumbusho ya Vijiji yaliyopo sehemu ya wazi yakionyesha makabila ya Tanzania na historia yao, vile vile Kanisa Kuu la Mt. Yosefu (St. Joseph’s Cathedral), Nyumba ya Utume ya Shirika la White Father, Bustani za Mimea, Ikulu ya zamani na masoko mengi ya kupendeza.
Tanzania inasifika kwa kuwa na mazingira ya asili na mbuga za wanyama za kupendeza na Hifadhi ya Baharini ya Kisiwa cha Bongoyo, kilichopo km 7 kaskazini mwa jiji, kimebarikiwa kwa kuwa na maeneo mazuri ya kuogelea na kupiga mbizi, vilevile fuo za kupendeza, visiwa vilivyojitenga na aina nyingi mbalimbali za viumbe wa baharini. Dar es Salaam pia ni lango kuu la kwenda Zanzibar, mkusanyiko wa visiwa vizuri katika Bahari ya Hindi. Huduma maarufu ya feri ya kwenda Kisiwa cha Zanzibar inapatikana upande wa pili wa barabara kutoka Johari Rotana.
Sasa Imefunguliwa
Gundua ulimwengu wa fahari na madaha hapa Johari Rotana, wenye machaguo ya malazi ya kisasa kabisa na yenye nafasi kubwa yakiambatana na starehe zisizokuwa na mpinzani, nyenzo za chakula na bisahara zinazokupa starehe kwa uzuri na urahisi.
Nyenzo za hoteli hujumuisha:
Vyumba na suite 193 na vyumba vya kupanga 60 vyenye huduma zote
Cigar Lounge yenye Cigar za kimataifa
Sehemu 3 maridadi za kula chakula, pamoja na huduma ya kula chakula chumbani
Intaneti yenye kasi ya juu ya fibre optic
Sehemu ya mazoezi ya viungo yenye vifaa vyote
Bwawa la kuogelea la nje
Sauna, vyumba vya mvuke na huduma ya kukanda mwili
Bwalo la hotelini kubwa zaidi nchini (mita za mraba 816)
Vyumba 6 vya mikutano vyenye vifaa vyote
Nyenzo za kufua nguo
Maegesho ya magari
Ulinzi wa saa 24
Huduma ya Daktari kwa muda wowote
Vyumba visivyoruhusu kuvuta sigara
Huduma ya kuhudumia watoto
Ziara za Jijini zinazoongozwa na waongoza watalii ambao ni wataalamu
Kukodi magari ya kifahari, kuchukuliwa uwanja wa ndege kwa kulipa ada
Johari Rotana inajali na kuthamini wateja wetu wenye uhitaji maalamu kwa kuhakikisha wanapata mazingira rafiki kulingana na mahitaja yao.
Huduma zinazopatikana:
Maegesho ya gari kwa kutumia Valet
Urahisi wa kuingia hotelini na viti vya walemavu
Lifti kubwa za kutoshea vizuri viti vya walemavu
Vyoo vya mahitaji maalum katika migahawa yote, vyumba vya mikutano, na maeneo mengine yote ya umma
Korido pana katika hoteli nzima
Maeneo yanayoweza kufikiwa kirahisi:
Kibo Lobby Lounge, Zafarani All Day Dining Restaurant, Hamilton's Gastropub
Tovuti hii inatumia vidakuzi ili tuweze kuboresha uzoefu wako wa mtumiaji na kupima utendaji wa tovuti yetu. Ikiwa utaendelea kutumia tovuti hii, utakuwa umekubali matumizi yetu ya vidakuzi.