Johari RotanaDAR ES SALAAMRRRRR
MUHTASARIMALAZICHAKULAMIKUTANO NA MATUKIOHARUSIBURUDANIVIFURUSHI NA OFATATHMINIPICHA
VYAKULA & BURUDANI

Sehemu mpya kabisa ya kula chakula jijini Dar es Salaam, inawapatia wageni wa hotelini na wakazi wa Jiji uzoefu wa kipekee wa uaandaaji wa chakula usioweza kusahaulika. Sehemu zetu nne za kitofuati zinakupeleke katika safari ya kipekee ya mapishi, kuanzia mapishi halisi ya Kichina ukiwa Noble House hadi kwenye bufee kubwa ya ladha za Kimediterania, Kihindi Kiarabu na Kiswahili ukiwa katika mgahawa wa siku nzima wa Zafarani. Kibo Lobby Lounge ni sehemu ya kufurahia kahawa yako au kinywaji cha starehe, huku Hamilton’s Gastropub ni kituo cha starehe kilichochangamka ambacho kitakuvutia kwa vyakula vya Kiingereza na Kimarekani.

Pata ofa na promosheni zetu za hivi karibuni kwenye Migahawa yetu yote kwenye kurasa zetu katika Rotana Times ]
HAMILTON’S GASTROPUB
Mapishi ya Kiuingereza na Kimarekani

TAZAMA PICHA
TAZAMA MENYU
TAZAMA OFA
WEKA NAFASI YA MEZA

Ufanye usiku wako uwe wa kukumbuka ukiwa Hamilton’s Gastropub mahali ambapo mapishi ni matamu na mazingira yanachangamsha. Menyu ya kuvutia ya vyakula vya Kiuingereza na Kimarekani vinatengenezwa kwa bashasha katika eneo hili lililochangamka kwa mapambo ya mtindo wa zama za kikoloni, viti vya kukaa vya nje na ndani na samani za kustarehesha.

Furahia muziki murua na vinywaji vinavyoandaliwa na kumiminwa kitaalamu katika baa hii ya kipekee Jijini Dar es Salaam inayokuhakikishia nyakati za furaha na chakula kizuri kuanzia mchana hadi usiku.

Eneo la kucheza watoto lililopo karibu na Hamilton's, linakuwezesha kustarehe na kufurahia kinywaji au mlo wakati watoto wako wanafurahia michezo.

Saa za Ufunguzi:
5.00 pm – 12 am

NOBLE HOUSE
Mapishi ya Kichina

TAZAMA PICHA
TAZAMA OFA

Kufunguliwa hivi karibuni

Furahia ladha halisi ya nchi za Mashariki ukiwa kwenye mgahawa wetu mahususi wa vyakula vya Kichina, Noble House; mahali ambapo wapishi wetu wa Kichina wamechagua aina mbalimbali ya vyakula halisi vyenye ladha nzuri ambazo zitakupeleka China bila kutoka Tanzania. Ukiwa na samani za kisasa, mwanga mtulivu na mapambo ya kupendeza ambayo yanaakisi ustadi wa kipekee na haiba ya Mashariki ya Mbali, unaweza kula chakula cha kipekee cha jioni ukiwa na familia, marafiki au wafanyakazi wenzako katika eneo hili mwandani la kulia chakula.

Saa za Ufunguzi:
Siku 7 kwa wiki, chakula cha jioni pekee. 17:30 - 23:00- siku za wiki na 17:30 – saa sita usiku mwishoni mwa wiki (Ijumaa - Jumapili)

ZAFARANI ALL DAY DINING
Mapishi ya Kimediterania, Kihindi Kiarabu na Kiswahili

TAZAMA PICHA
TAZAMA MENYU
TAZAMA OFA
WEKA NAFASI YA MEZA

Una uchaguzi mwingi wa vyakula ukiwa Zafarani, mgahawa wetu wa kisasa wa siku nzima ambapo wapishi wetu wenye vipaji vya hali ya juu wanaandaa vyakula vinavyovutia na mapishi ya Kimediterania, Kihindi, Kiarabu na Kiswahili. Wageni wanaweza kujaribu ladha za vyakula kutoka duniani kote wakati wa kifungua kinywa, chakula cha mchana na cha jioni katika eneo hili la kustarehesha lenye mwanga mtulivu. Chagua kutoka kwenye bufee kubwa au chagua chakula unachokipenda kutoka kwenye menyu yetu ya a la carte.

Saa za Ufunguzi:
Kifungua Kinywa: 6.30 am – 10.30 am
Chakula cha Mchana: 12:00 pm - 2:30 pm
Chakula cha Jioni: 6:00 pm - 10:00 pm

KIBO LOBBY LOUNGE
Vinywaji, vyakula vyepesi, vitobosha na vitindamlo

TAZAMA PICHA
TAZAMA MENYU
TAZAMA OFA

Kaa kwenye kiti na tazama dunia ikiendelea ukiwa Kibo Lobby Lounge, sehemu iliyotengenezwa kifahari ikiwa na mwanga tulivu na mapambo ya kisasa. Panafaa kwa mikutano isiyo rasmi na wafanyakazi wenzako au wateja wako au kwa mikutano na marafiki au familia mkiburudika na chai au kahawa na vitobosha. Mgahawa wetu unakupatia maeneo kadhaa ya kukaa yenye faragha ambapo unaweza kufanya mazungumzo au mikutano ya kawaida. Vitindamlo vitamu, vyakula vyepesi, na vinywaji vinavyoburudisha pia vinapatikana kwenye menyu inayotamanisha.

Saa za Ufunguzi:
7.00 am – 11.00 pm

HUDUMA YA CHAKULA CHUMBANI
Mapishi ya Kimataifa

TAZAMA PICHA
TAZAMA MENYU

Wageni wanaweza kufurahia mapishi yanayoandaliwa Johari Rotana huku wakiwa chumbani mwao, kwenye suite au chumba cha kupanga, kwa kuchagua miongoni mwa mapishi mbalimbali ya kimataifa kutoka kwenye menyu yetu ya huduma ya chakula chumbani.

Kuanzia kitafunio au kiburudisho cha usiku wa manane hadi mlo binafsi ukijumuika pamoja na marafiki na familia, tunaweza kukuandalia vyakula unavyovipenda na kukuletea chumbani kwako. Wewe tupigie tu simu na tutafurahia kukusaidia.

Saa za Ufunguzi:
Saa 24 kila siku, siku 7 za wiki

THE CIGAR LOUNGE
Classic British

TAZAMA PICHA

Ukumbi wa Cigar wa kifahari ulioundwa kwa ajili ya wapenzi wa Cigar kufurahia mchanganyiko bora katika mazingira yenye utulivu na staha.

Saa za Ufunguzi:
Jumatatu -Jumapili: 4:00 PM - 1:00 AM

KUHUSU ROTANATOVUTI ZA ROTANA
HISTORIA
MAADILI YA ROTANA
DIRA / AHADI YA CHAPA
TUZO ZETU
BODI YA WAKURUGENZI
WATENDAJI WA SHIRIKA
MAENDELEO YA HOTELI
NAFASI ZA KAZI ZINAZOKUJA
ALAMA YA CHAPA
WASHIRIKA WA TASNIA
ROTANA DUNIA/ WAJIBU WA SHIRIKA KWA JAMII (CSR)
CHUMBA CHA HABARI
MATANGAZO NA VYOMBO VYA HABARI
MAKTABA YA PICHA NA VIDEO
OFISI ZA MAUZO NA GDS
WAGENI WA MASHIRIKA
www.rotana.com
www.rotanatimes.com
www.rotanaearth.com
www.rotanacareers.com
© Hakimiliki 2024 Shirika la Usimamizi wa Hoteli Rota PJSC.
Tafadhali angalia
Masharti yetu ya Matumizi
Sera ya Faraghaolicy
Cookie Settings
Tovuti hii inatumia vidakuzi ili tuweze kuboresha uzoefu wako wa mtumiaji na kupima utendaji wa tovuti yetu.
Ikiwa utaendelea kutumia tovuti hii, utakuwa umekubali matumizi yetu ya vidakuzi.
Soma Tamko la Kidakuzi
KUBALI